Home news PACHA WA CHAMA AMFANYA PABLO ‘KUCHEKELEA KOONI’…ASEMA SASA NI KAZI KAZI..AMGUSIA MZAMIRU…

PACHA WA CHAMA AMFANYA PABLO ‘KUCHEKELEA KOONI’…ASEMA SASA NI KAZI KAZI..AMGUSIA MZAMIRU…


PABLO Franco, Kocha wa Simba amefunguka kuwa kurejea kwa viungo wake Rally Bwalya na Mzamiru Yassin kumeongeza nguvu na ari ya kufanya vizuri zaidi katika ratiba yao ngumu.

Timu hiyo itacheza mechi tatu mfululizo ndani ya siku 10, ambapo Ijumaa walianza ratiba hiyo kwa kucheza na Biashara United kisha dhidi ya Dodoma Jiji Machi 7, na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane Machi 17.

Bwalya ambaye amekuwa akitumika kucheza pacha kwenye kiungo cha timu hiyo na Clatous Chama hakuwepo katika timu hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia.

Pablo alisema: “Tumekuwa na ratiba ya michezo mitatu migumu na muhimu dhidi ya Biashara United, Dodoma Jiji na RS Berkane, kwa kuwa michezo hii ni ya mfululizo, tunahitaji kuwa na kikosi chetu kamili na wachezaji wote muhimu.

“Nafurahi kuona tayari Mzamiru na Bwalya wakirejea kujiunga na wenzao baada ya kushindwa kusafiri nasi kwenye Kombe la Shirikisho, katika kipindi ambacho tunakabiliwa na majeruhi kurejea kwao ni wazi kumetuongezea nguvu ya kufanya vizuri zaidi.

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA KAMILI NA TEREHE KWA MECHI ZA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA...