Home Habari za michezo FT: SIMBA 2-0 SINGIDA FG…..ONANA KAMA RONALDO….MIQUISSONE MPYAAAAA…

FT: SIMBA 2-0 SINGIDA FG…..ONANA KAMA RONALDO….MIQUISSONE MPYAAAAA…

FT:SIMBA 2-0 SINGIDA FG

Mchezo wa pili kwa Simba wa Kombe la Mapinduzi uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex umemalizika kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini safu za ulinzi zilikuwa imara kuhakikisha nyavu zao haziguswi.

Willy Onana aliipatia Simba bao la kwanza dakika ya 46 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18.

Luis Miqussone aliifungia Simba bao la pili kwa shuti kali la mguu wa kushoto dakika ya 58 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

X1: Ally, Kapombe, Israel, Kennedy, Che Malone, Abdallah (Mussa 45:)(Chilunda 81′), Phiri (Miqussone 45′), Kanoute, Bocco (Baleke 45′), Ngoma, Onana (Karabaka 81′)

Walioonyeshwa kadi: Ally 72′ Mohamed Mussa 76′ Kanoute 83′

X1: Ibrahim, Kijili, Mbegu (Kadikilo 68′), Onyango, Carno, Kagoma, Kaseke, Chukwu, Rupia (Ambundo 68′), Kyombo (Kazadi 68) , Abuya (Kagere 68′)

Walioonyeshwa kadi: Kyombo, Kijili 50′ Mbegu 68′ Carno 80′

SOMA NA HII  BANGALA AMKINGIA KIFUA FEI TOTO