Home Uncategorized UJUMBE HUU WATUMWA KAGERA SUGAR KUTOKA SIMBA

UJUMBE HUU WATUMWA KAGERA SUGAR KUTOKA SIMBA


JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa wataendelea kuzitafuta pointi tatu kwenye mechi zao zote watakazocheza ikiwa ni pamoja na mechi ya kesho dhidi ya Kagera Sugar.

Simba itaikaribisha Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara baada ya ule wa kwanza kushinda kwa mabao 3-0.

“Tunakazi kubwa ya kutafuta pointi tatu kwenye mechi zet za ligi, tunaoma mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kazi yetu uwanjani inawategemea mashabiki,” amesema.

Bocco ametupia jumla ya mabao matatu na pasi moja ya bao ndani ya Simba iliyofunga jumla ya mabao 46.

SOMA NA HII  KISA CORONA...SHIBOUB ASUBIRI RUHUSA YA RAIS SUDANI KURUDI TZ..!!