Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA NA KIBABAGE…..MAJEMBE MENGINE YANGA KUTUA KWA STAILI HII…

BAADA YA KUANZA NA KIBABAGE…..MAJEMBE MENGINE YANGA KUTUA KWA STAILI HII…

Tetesi za usajili Yanga

Uongozi wa Yanga umesitiza juu ya kumalizana na wachezaji wote ambao walikuwa wakiwahitaji, huku wakiweka wazi kuwa hakuna mchezaji mwingine yeyote ambaye walikuwa wanamhitaji ambaye hawajamalizana naye.

Yanga mpaka sasa tayari wamemtambulisha mchezaji mmoja, mzawa winga Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate alikokuwa kwa mkopo akitokea Mtibwa Sugar huku kwa wachezaji wa kigeni wakiwa bado hawajaanza kazi.

Yanga wanahusishwa kukamilisha usajili wa wachezaji wengine kama Maxi Mpiana kutoka DR Congo, Aubin Kramo kutoka Ivory Coast, Jonas Mkude aliyeachwa na Simba na Mohamed Zougrama kutoka Asec Mimosas.

Akizungumza nasi, Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji alisema kuwa wao kama uongozi tayari walishakamilisha usajili wa wachezaji wote ambao walikuwa wakiwahitaji hivyo hakuna mchezaji mwingine ambaye wanamfukuzia kwa sasa.

“Yanga tayari tumekwisha maliza taratibu zote za kuwasajili wale wachezaji wote ambao tulitaka kuwasajili kwa msimu huu hivyo hakuna mchezaji mwingine yeyote ambaye tunamhitaji na tunamfuatilia.

“Kwa sasa ambacho tunakifanya ni kuhakikisha kuwa tunafuata taratibu zetu za utambulisho kupitia kitengo chetu cha habari na mawasiliano, kwani ndio jambo ambalo linafuata muongozo wa kiofisi na makubaliano ya ukuaji katika sekta hiyo ya habari ya Yanga,” alisema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO 'UCHAWI' WA CHAMA ULIVYOWARUGA WAZAMBIA WENZAKE LEO....KAZI HAIKUWA RAHISI..