Home Habari za michezo NGOWI:- JEZI ZA YANGA KWA MISIMU MITANO IJAYO ZIKO TAYARI…..

NGOWI:- JEZI ZA YANGA KWA MISIMU MITANO IJAYO ZIKO TAYARI…..

Habari za Yanga

Mbunifu maarufu wa mavazi nchini ambaye amekuwa akibuni jezi za Klabu ya Yanga, Sheria Ngowi amesema kuwa tayari ameshamaliza kubuni na kuandaa jezi za misimu mitano ijayo.

Kauli hiyo ya Ngowi ameitoa wakati akihojiwa na Clouds FM ikiwa ni saa chache baada ya Yanga kuachia uzi mpya kwa ajili ya michuano ya Kimataifa ya CAFCL itakayoanza kesho huku akisema kuwa anasubiri uongozi wa Yanga upitishe tu.

“Sifikirii kufanya kazi na klabu nyingine, nimeamua hilo kwa sababu naheshimu riziki Yangu ndani ya Yanga.

“Tayari jezi za misimu mitano mbele za Yanga nimeshamaliza kuzibuni na ninachosubiri kwa sasa ni ruhusa Kwa viongozi nizitoe muda ukiwadia,” amesema Ngowi.

SOMA NA HII  MWAKINGWE: SIWADAI WACHEZAJI, KILICHOTOKEA TANGA KILA MTU AMEONA