Home Uncategorized MAJIMAJI:TUNAIFUNGA SIMBA KESHO KWA MKAPA

MAJIMAJI:TUNAIFUNGA SIMBA KESHO KWA MKAPA

 


UONGOZI wa Majimaji umeweka wazi kuwa kesho utaingia ndani ya uwanja ukiwa na lengo moja la kupata matokeo mbele ya Simba.

Desemba 27, Simba itawakaribisha Majimaji ya Songea kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo ni wa hatua ya tatu na atakayepoteza atafungashiwa virago jumlajumla na mshindi atatinha hatua ya nne ya Kombe la Shirikisho.

Simba ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambapo walitwaa baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Majimaji, Godfrey Mvula amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao ila wataingia ndani ya uwanja kwa lengo la kusaka ushindi.

“Tunatambua kwamba Simba ni timu kubwa hilo lipo wazi lakini wanakutana na timu kubwa pia kwani nasi pia tupo kwenye ligi kwa muda mrefu.

“Tunashiriki Ligi Daraja la Kwanza, ushindani uliopo huku ni mkubwa hivyo tunaamini kwamba tunao uwezo wa kushinda mbele ya wapinzani wetu hilo linawezekana.

“Wachezaji wana morali kubwa na kila mmoja anatambua kinachohitajika ni ushindi hakuna kitu kingine hivyo wajitokeze kutupa sapoti,” .


Kabla haijashuka Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18, Majimajili, mchezo wake wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea ngoma ilikamilika kwa kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  SIMBA: TUTAFANYA VIZURI MBELE YA FC PLATINUM