Home Uncategorized YANGA WAANZA KUIVUTIA KASI TANZANIA PRISONS

YANGA WAANZA KUIVUTIA KASI TANZANIA PRISONS

 


KIKOSI cha Yanga leo Desemba 26 kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 31, Uwanja wa Nelson Mandela ni wa mzunguko wa pili.


Yanga inakutana na Prisons ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 bila kupoteza. Imeshinda mechi 13 na kukusanya sare tatu.

Kwa upande wa Tanzania Prisons ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 imekusanya pointi 21 ipo nafasi ya 11.


Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa malego yao ni kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao ujao ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Haitakuwa kazi rahisi ila tupo tayari kwa ajili ya kuendeleza ushindani ndani ya ligi. Wachezaji walipata mapumziko kwa ajili ya Christmas ila leo Desemba 26 wanaanza maandalizi.

“Mchezo wetu utakuwa ni Alhmasi ila kwa sasa tupo Mbeya kuhusu kuondoka utaratibu utawekwa wazi,” .

SOMA NA HII  HIZI HAPA DAKIKA 450 ZA MOTO KWA MBELGIJI WA YANGA, RATIBA YAKE BALAA, BANDIKA BANDUA