Home Simba SC KIGOGO SIMBA AFUNGUKIA ISHU YA AFRICAN SUPER LEAGUE

KIGOGO SIMBA AFUNGUKIA ISHU YA AFRICAN SUPER LEAGUE


MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa Uongozi wa klabu hiyo unajivunia kuwa sehemu ya ushirikishwaji katika mchakato wa kuanza kwa michuano mikubwa ya African Super League.

Michuano hiyo ambayo mwanzo ilitokana na pendekezo la Rais wa Shirikisho la soka duniani, Gian Infantino ambaye alipendekeza kuanzishwa kwa ligi hiyo itakayokuwa na timu 20 za kudumu, huku pia kukiwa na timu ambazo zitakuwa zikipambana kusaka nafasi ya kucheza michuano hiyo.

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe hivi karibuni amesema: “Wamejifunza mengi kuhusu jaribio la Super League ya Ulaya ambalo lilifeli, na ana matumaini makubwa kuwa, kutokana na kujifunza huko watafanikiwa katika mpango wa African Super League.

Akizungumzia kuhusu mpango huo, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema: “Kuhusiana na michuano ya Super League, ni ngumu kuzungumza kitu kwa sasa kwa kuwa tupo katika hatua za awali za mazungumzo juu ya hilo.

“Kwa sasa hatuwezi kusema tumefikia katika hatua gani kwa kuwa kama ambavyo nimesema tupo katika hatua za awali, na tutatoa taarifa zaidi pale mchakato utakapokamilika, lakini kama uongozi wa Simba tunajivunia kuwa sehemu ya mchakato huu, hii bila shaka inaonyesha ukubwa ambao kama timu tunao.”

SOMA NA HII  BENCHIKHA AWAPIGA MKWARA MASTAA WANAOCHEZA 'KIFAZA FAZA' SIMBA...