Home Habari za michezo KISASI CHA 5G KULIPWAAA!!?…..TFF WAZIKUTANISHA TENA SIMBA NA YANGA….

KISASI CHA 5G KULIPWAAA!!?…..TFF WAZIKUTANISHA TENA SIMBA NA YANGA….

Habari za michezo

Kikosi cha timu ya wanawake cha Yanga, Yanga Princess kinatarajiwa kucheza dhidi ya Simba Queens katika mchezo wa Ngao ya Jamii Wanawake hatua ya nusu fainali.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Yanga Princess itapambana na Simba Queens Desemba 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mshindi wa mechi hiyo atacheza fainali dhidi ya mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya JKT Queens na Fountain Gate Princess.

Mechi hizo za Ngao ya Jamii, ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake 2023-2024.

Fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake itachezwa Desemba 12, 2023, kabla ya mchezo huo wa fainali, mapema itapigwa ya kumsaka mshindi wa tatu. Mechi zote hizo zitachezwa Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  JINSI DAKIKA 360 ZA AUCHO ZINAVYOMTESA MUKOKO YANGA..KIGOGO TFF ASHINDWA KUJIZUIA ..AFUNGUKA..