Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA ASEC ….MASTAA HAWA SIMBA WAPEWA ‘HIRIZI’ ZA MCHEZO MAPEMAAA….

KUELEKEA MECHI NA ASEC ….MASTAA HAWA SIMBA WAPEWA ‘HIRIZI’ ZA MCHEZO MAPEMAAA….

Habari za Simba leo

Kuelekea kwenye mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas nyota wa Simba wamepewa zigo zito kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwenye mchezo huo.

Ipo wazi kuwa katika mechi mbili zilizopita za ligi wachezaji wa Simba walipata matokeo yenye maumivu. Katika mchezo wa Kariakoo Dabi Novemba 5 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga na mchezo mwingine Simba 1-1 Namungo.

Ni Che Malone Fondoh beki wa kazi alikuwa shuhuda kwenye mechi hizo mbili wakiokota mabao sita kwenye ligi nyavuni huku Moses Phiri akiwa shuhuda safu ya ushambuliaji ikifunga mabao mawili ndani ya dakika 180.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameliambia Championi Jumatano kuwa wachezaji wote wanatambua kazi nzito iliyopo ni kupata matokeo dhidi ya ASEC Mimosas.

“Kazi kubwa ipo kwenye mechi zetu zote na wachezaji wanatambua namna hali ilivyo. Kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zilizopita hilo litabaki hivyo halitabadilika lakini kupata matokeo kwa mechi zijazo lipo ndani ya uwezo wao.

“Kujitoa na kutimiza majukumu kwa wakati hilo ni muhimu. Tunaamini wachezaji waliopo wana kazi kubwa kutafuta matokeo dhidi ya ASEC Mimosas hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya mchezo wetu muhimu,” alisema Ally.

Ipo wazi kuwa mchezo wa mwisho Simba kucheza Uwanja wa Mkapa ilikuwa Novemba 5 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga.

SOMA NA HII  MKWAKWANI PATASHIKA NGUO KUCHANIKA...WACHEZAJI WATALISHWA UDUVI...WATAOGESHWA MAJI YA IRIKI