Home Uncategorized SIMBA YAIPOTEZA MAZIMA YANGA

SIMBA YAIPOTEZA MAZIMA YANGA


SAFU ya ushambuliaji ya Simba iliyo chini ya Meddie Kagere imevunja rekodi ya mabao yaliyofungwa na Yanga msimu uliopita 2018/19.

Yanga ilimaliza Ligi ikiwa imefunga mabao 56 ambayo kwa sasa Simba imeipoteza kabla ya Ligi Kuu Bara kumalizika.

Safu ya ushambuliaji ya Simba kwa sasa imetupia mabao 63 ambayo ni mengi kuliko timu zote zinazoshiriki ligi kwa sasa.

Rekodi ya kibabe inayowindwa na Simba kwa sasa ni Ile ya Yanga iliyowekwa msimu wa 2015/16 kwa kumaliza ligi na mabao 70 pia kuvunja rekodi waliyoiweka msimu wa 2018/19 kutupia mabao 77.


Simba inaongoza ligi kwa sasa ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi 63 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 51.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI