Home Uncategorized LUSAJO AJIPA MUDA WA WIKI MOJA KABLA YA KUANZA KUJINOA

LUSAJO AJIPA MUDA WA WIKI MOJA KABLA YA KUANZA KUJINOA


NYOTA wa timu ya Namungo, Reliants Lusajo amesema kuwa kwa sasa amejipa muda wa wiki moja kupumzika kabla ya kuanza mazoezi ya kulinda kipaji chake.

Lusajo ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia mabao 11 na ametoa pasi tatu za mabao jambo linalimfanya awe miongoni mwa wazawa walio ndani ya tano bora kwa utupiaji.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Lusajo amesema kuwa: “Kwa sasa bado nipo nimepumzika nina mpango wa kuanza kufanya mazoezi baada ya kumaliza wiki moja.

“Inabidi nipumzike ukizingatia kwamba muda mwingi tulikuwa na mechi ngumu na zenye ushindani muda huu uliopo lazima nipumzike kabla ya kurejea kwenye mazoezi,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA