Home Uncategorized KOCHA COASTAL UNION AWAPA KAZI YA KUFANYA WACHEZAJI WAKE

KOCHA COASTAL UNION AWAPA KAZI YA KUFANYA WACHEZAJI WAKE

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa wachezaji wake ni lazima wafanya mazoezi ili kulinda uwezo wao walionao kwenye soka.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali ilisitisha shughuli zote zinazohusu mjumuiko kwa muda wa mwezi mmoja.

“Kila mchezaji amepewa jukumu la kufanya ambapo ni lazima wote wazingatie mazoezi ili kulinda uwezo wao kwani ni lazima kulinda vipaji vyao ili kuwa bora.

“Pia nimewaambia wanapaswa wachukue tahadhari kwani Virusi vya Corona sio vya kuchukulia utani,” amesema Mgunda.

Coastal Union ipo nafsi ya tano kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 46. 

SOMA NA HII  NAMUNGO WANAFANYIA KAZI MAKOSA YAO VPL