Home Uncategorized KIPA BIASHARA UNITED AWA BIASHARA KWA MATAJIRI WA BONGO NA KMC

KIPA BIASHARA UNITED AWA BIASHARA KWA MATAJIRI WA BONGO NA KMC

DANIEL Mgore kipa namba moja ndani ya Klabu ya Biashara United inaelezwa kuwa amewekwa kwenye rada za Klabu ya KMC na matajiri wa Dar, Azam FC.

Mgore ni miongoni mwa makipa makini ndani ya Uwanja ambapo amemuaminisha Kocha Mkuu, Francis Baraza kuwa anaweza kazi.

Azam FC wanahitaji kipa atakayekuwa mbadala wa Razack Abarola ambaye mkataba wake unameguka mwishoni mwa msimu na bado hajaongeza mwingine.

KMC inaelezwa kuwa wapo kwenye mkakati wa kuboresha kikosi chao ambapo inatajwa kuwa kuna hatihati Jonathan Nahimana ambaye ndiye mlinda mlango namba moja anaweza kuwa biashara kwenye timu nyingine msimu ujao baada ya kuzivutia timu mbalimbali za Bongo na nje ya Bongo

Biashara United ipo nafasi ya 10 ikiwa imecheza mechi 29 imefungwa mabao 22 huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 21 kibindoni ina pointi 40.

SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA BARCELONA SETIEN MAMBO MAGUMU