Home Uncategorized MABEKI HAWA CHIPUKIZI WAPELEKWA DARASANI NA KIRAKA ERASTO NYONI

MABEKI HAWA CHIPUKIZI WAPELEKWA DARASANI NA KIRAKA ERASTO NYONI

ERASTO Nyoni kiraka wa Simba ni miongoni mwa wakongwe ambao muda wote ndani ya uwanja wanafanya vema huku wakiwapeleka darasani mabeki chipukizi wanaokipiga klabu nyingine.

Kennedy Juma ambaye naye anakipiga ndani ya Simba ni miongoni mwa mabeki ambao wanakubali uwezo wa Nyoni.

Dickson Job beki chipukizi anayekipiga ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar amesema kuwa amekuwa akizitazama video za mechi zao dhidi ya Simba huku akijifunza mengi kutoka kwa mkongwe Nyoni.

Bakari Mwamnyeto beki anayekipiga ndani ya Klabu ya Coastal Union naye ni miongoni mwa wanafunzi wa Nyoni ambapo amesema anavutiwa na utendaji wa kazi pamoja na maelekezo yake. “Ni mtu wa kazi ndani ya uwanja hapendi utani hata kidogo muda wote anatoa maelekezo na kufuatilia huku naye akitimiza, pale unapokosea anakuelekeza ili uwe bora, ni darasa tosha kwangu,” amesema Mwamnyeto ambaye alicheza na Nyoni timu ya Taifa ya Tanzania.

SOMA NA HII  KIRAKA MPYA WA YANGA APEWA MITIHANI MITATU CHAP