Home Habari za michezo WAKATI MPOLE NA BANGALA WAKILIA LIA KILAINI LAINI TU…HIVI NDIVYO MBRAZILI WA...

WAKATI MPOLE NA BANGALA WAKILIA LIA KILAINI LAINI TU…HIVI NDIVYO MBRAZILI WA SINGIDA ‘ANAVYOCHINJWA’ KILA SIKU…


Wakati mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, George Mpole akilalamika kutofunga goli mpaka sasa katika mechi mbili za mwanzo wa Ligi kutokana na kukamiwa na mabeki na kuchezewa ndivyo sivyo.

Bado kuna wengi wanalalamika kitendo cha Mtenje Albano wa Coastal Union kuoneshwa kadi ya njano badala ya nyekundu kwa kitendo cha kudhamiria kumuumiza nyota wa Yanga Yannick Bangala.

Wakati huo huo usisahau lawama alizopelekewa beki wa Simba Henock Inonga Baka kwa mchezo usio wa kingwana dhidi ya Sure boy.

Sasa yote tisa, pichani ni miguu ya Kiungo fundi wa Kibrazil anayekimbiza vilivyo katika timu ya Singida Big Stars Dario Frederico, ambayo inaonesha ni namna gani anavyotembezewa kiatu.

Dario Federico amecheza michezo miwili ya Ligi mpaka sasa na ameonesha uwezo mkubwa pengine ndio sbabu ya kuchezewa rafu na wachezaji wa timu pinzani.

Vitendo visivyokuwa vya kiungwana vimewaibua baadhi ya Makocha wa vilabu vya Ligi Kuu ambao wametoa rai kwa wachezaji kulindania.

SOMA NA HII  PACOME:- MECHI NA AL AHLY DUA ZENU ZINAHITAJIKA SANA....NI WAGUMU MNOO..