Home Habari za michezo BAADA YA KUSAJILIWA NA MAJERUHI KAMA YOTEE…KAMBOLE AANZA KUNYANYUKA YANGA…KAPEWA MECHI NA...

BAADA YA KUSAJILIWA NA MAJERUHI KAMA YOTEE…KAMBOLE AANZA KUNYANYUKA YANGA…KAPEWA MECHI NA AZIZ KI…


Kurejea kwa mshambuliaji Mzambia Lazarous Kambole kumemlazimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi kutengeneza kombinesheni mpya ya ushambuliaji hatari.

Kambole amerejea uwanjani juzi na kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake huko kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambako wameweka kambi.

Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, alisema kuwa mara baada ya Kambole kurejea uwanjani, kocha ameonekana akiijaribu kombinesheni yake na kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki.

Aliongeza kuwa kocha huyo ameonekana kuvutiwa na Kambole mazoezini kutokana na kiwango bora cha kufunga mabao ambacho amekionyesha akiwa ndani na nje ya 18. “Tuna jumla ya washambuliaji watatu katika timu, ambao wote anakubali uwezo wao kutokana na umahiri mkubwa wa kufunga mabao walionao uwanjani.

“Hivyo basi anajaribu kutengeneza kombinesheni tofauti za ushambuliaji, mara kadhaa amekuwa akimchezesha Mayele, Makambo wote wakicheza namba 9 lakini nyuma yao anakuwepo Aziz Ki. “Lakini juzi mara baada ya Kambole kurejea uwanjani na kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake, ameonekana akimchezesha pamoja na Aziz Ki.

“Kwa maana ya Kambole kucheza namba 9 na Aziz Ki 10, kocha huyo anaitengeneza kombinesheni hiyo mpya ya ushambuliaji kwa lengo la kusuka kikosi imara ambacho hakitamtegemea mchezaji mmoja pekee katika timu,” alisema bosi huyo.

SOMA NA HII  WAKATI TETESI ZA MAYELE KUTAKIWA NA KAIZER CHIEFS ZIKIZIDI KUKUA...INJINIA HERSI AIBUKA NA HILI JIPYA....