Home Habari za michezo ISHU YA UWEKEZAJI MO DEWJI NA SIMBA YAFIKA BUNGENI…”MWEKEZAJI ANALETA JANJA JANJA

ISHU YA UWEKEZAJI MO DEWJI NA SIMBA YAFIKA BUNGENI…”MWEKEZAJI ANALETA JANJA JANJA

ISHU YA UWEKEZAJI MO DEWJI NA SIMBA YAFIKA BUNGENI...

Siku moja baada ya Mwanachana na Shabiki wa Simba SC Ally Mikoi ‘Kisugu’ kumtaka Mbunge wa Makete Festo Sanga kuacha
kuizungumzia Simba SC vibaya, Mbunge huyo ameibuka na kumjibu Kisugu.

Mbunge Sanga amesema haishambulii Simba SC kama
inavyozemwa na wengi na kuongeza ni mapenzi yake dhidi ya timu hiyo.
“Mwenendo wa Klabu yetu ya Simba ambayo ninaishabikia sio mzuri, kwa heshima, kwa hadhi, kwa umri na kwa namna ambavyo tunaijua na inavyoenda kwa sasa hairidhishi na mwenendo huu ni matokeo ya vitu flani.

“Kwanza ni aina ya uongozi unavyoendesha mambo yake na pili ni aina ya uwekezaji na mwekezaji mwenyewe anavyo-behave ndani ya klabu. Kwenye Taifa letu kuna Yanga na Simba, zinatambulisha taifa letu kisoka, zote zimeamua kutoka kwenye community based club kwenda kwenye mfumo wa kampuni.

“Wenzetu Yanga wanafanya mchakato wa mabadiliko ambao na sisi Simba tunafanya, lakini sisi Simba tuna ukata, mwekezaji haeleweki, akijitokeza kwenye media anasema timu inampa hasara, kama anakula hasara kuna haja gani ya kuendelea kuikumbatia hiyo timu? Akijitokeza anasema ameinunua timu, sisi tunachojua Simba haijaingia kwenye soko la hisa, hizo hisa zilinunuliwa linin a zilinunuliwa shilingi ngapi?

“Ili tuinusuru Simba lazima kwanza tukubali kuwa timu ina changamoto na mashabiki tuwaambie ukweli. Kuugulia mioyoni sio suluhisho la kutibu matatizo yetu, tuseme ukweli changamoto zipo, timu haina hela, mwekezaji analeta janja janja kwenye klabu yetu ya Simba, kama anapata hasara anaweza akapisha wawekezaji wengine wakaingia na timu ikarudi kwenye hadhi yake,” amesema Sanga.

SOMA NA HII  BACCA AMGEUKIA JOB YANGA...KUMBE WAMERUHUSU GOLI MOJA TU...LIST KAMILI HII HAPA