Home Habari za michezo BAADA YA SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA SASA NI ZAMU YA...

BAADA YA SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA SASA NI ZAMU YA BANDA AKIMBILIA HUKU

Beki wa Tanzania, Abdi Banda anayecheza Afrika Kusini, ameweka wazi kinachoendelea kati yake na klabu ya Chippa United, baada ya hivi karibuni kutumiwa barua ya kuvunjiwa mkataba.

Banda aliingia mgogoro na klabu hiyo baada ya kuitwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mei mwaka huu na Chippa ilimtaka kupunguza mshahara wake kuanzia Juni Mosi jambo ambalo ameligomea.

Banda amesema kitendo cha kukataa kupunguziwa mshahara ndicho kilichosababisha waajiri wake kusitisha mkataba na kukimbilia FIFA.

“Sijaweza kukubaliana nao kwa sababu hatukujadiliana, sasa baada ya kuona wanaleta mambo ambayo sijakubaliana nayo, niliamua kufungua kesi FIFA ili nikapate haki yangu,” amesema.

Aidha Banda ameongeza bado ana mkataba wa mwaka mmoja uliobaki na klabu hiyo na wakati kesi hiyo ikienda kusikilizwa atarudi Afrika Kusini kutafuta timu kabla ya maamuzi hayo.

Katika barua ya FIFA iliyotolewa kuhusu sakata hilo, Chippa imetakiwa kuwasilisha utetezi wao kuhusu kesi hiyo Julai 18, huku hukumu ikitarajiwa kutolewa rasmi Septemba 18 mwaka huu.

Ikiwa Banda atashinda kesi hiyo inayosimamiwa na mwanasheria wake, Lyrique de Plessis raia wa Ungereza basi Chippa itabidi imlipe fidia ya Randi4.5 milioni ambazo ni wasa na Sh600 milioni.

SOMA NA HII  FEI TOTO:- GSM ANAINGIZA PESA KWA KIPAJI CHANGU...ANADHARAU SANA YULE...