Home Habari za michezo FEI TOTO:- GSM ANAINGIZA PESA KWA KIPAJI CHANGU…ANADHARAU SANA YULE…

FEI TOTO:- GSM ANAINGIZA PESA KWA KIPAJI CHANGU…ANADHARAU SANA YULE…

Habari za Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema kuwa mdhamini wa klabu hiyo, Ghalib Said Mohammed (GSM) amekuwa akimdharau ikiwa ni pamoja na kutopokea simu zake wala kujibu ujumbe wake wa simu.

Fei Toto amesema hayo wakati akihojiwa na Clouds FM huku akiongeza kuwa licha ya kufanyiwa vitendo visivyostahili na uongozi wa Yanga lakini wamekuwa hawana fadhira kwake kwani kipaji chake ndicho kinampa pesa bosi huyo wa GSM.

“Kipindi mgogoro huu unaanza mimi nilimtafuta Ghalib (GSM), nampigia simu zangu hapokei, namtumia meseji hazipokelewi, lakini nilipoamua kufanya maamuzi ndipo akaanza kunipigia simu, je, laiti ingekuwa ni wewe ungepokea? Hizi si dharau.

“Hata kama wewe ni tajiri lakini dharau sio kitu kizuri kwa sababu kipaji changu ndicho kinachokuingizia pesa wewe,” amesema Fei Toto.

Ikumbukwe kuwa, Fei Toto ana mgogoro na klabu yake ya Yanga ambapo ameshaandika barua ya kuomba kuondoka licha ya uongozi wa klabu hiyo kumuwekea ngumu, hivyo kwa sasa anasaka pesa ili akafungue shauri CAS.

SOMA NA HII  RASMI...ISHU YA MNIGERIA NA SIMBA IMEISHA..KAMA KAWA BARBARA ASISITIZA SAPRAIZI INAKUJA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here