Home news YANGA:TUNA UKUTA WA BERLIN,YATAMBA NA VIUNGO PIA

YANGA:TUNA UKUTA WA BERLIN,YATAMBA NA VIUNGO PIA


 UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba umesajili wachezaji chuma jambo ambalo linawafanya wawe na ukuta mgumu kama wa Berlin huku eneo la viungo ikiwa kazi ni kubwa.

Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli aliliambia Spoti Xtra kuwa dhamira kubwa ya kufanya usajili makini ni kuwa na chaguo la kufanya kwenye kila mechi ili wapate pointi tatu.

“Unaona kwamba kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar eneo la beki wa kati hakuanza Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha lakini ilikuwa kama hakuna kilichotokea kazi ilifanyika na tukapata ushindi.Tuna ukuta kama ule wa Berlin.

“Kwa upande wa viungo hakuwepo Tonombe Mukoko kwa sababu ana ile adhabu aliyopewa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii lakini bado eneo la kiungo lilisumbua  na kufanya vizuri.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga alibainisha kuwa uwezo wa ingizo jipya katika eneo la ulinzi Litombo Bangala ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa jambo linalomshangaza kila anapomtazama.

“Unakuwa na mchezaji mwenye uwezo mkubwa kama Bangala unadhani unahitaji nini kingine kama sio ushindi? Aina ya wachezaji wenye uwezo mkubwa kila mapigo kwake ni sahihi yupo yule Khalid Aucho huyu ni mzee wa pasi za uhakika kuna burudani kweli Yanga,” alisema Manara.

SOMA NA HII  HASSAN DILUNGA 'APIGWA KISU' AFRIKA KUSINI....ISHU NZIMA IKO HIVI...PABLO ATOA KAULI...