Home Uncategorized TSHISHIMBI AICHOKONOA YANGA KUHUSU MKTABA WAKE

TSHISHIMBI AICHOKONOA YANGA KUHUSU MKTABA WAKE

PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hajaongeza mkataba ndani ya klabu yake hiyo hivyo yupo huru kuzungumza na timu yoyote itakayokuwa ikimhitaji.

Nahodha huyo ambaye msimu uliopita ilielezwa kuwa Simba wanahitaji saini yake kwa sasa amebakiza kandarasi ya miezi minne ndani ya Yanga.

Kauli hiyo ni sawa na kuwachokonoa kimtindo mabosi wake hao ili wampe mahitaji yake kwani amesema anachohitaji ni dau la kuendeshea maisha yake.

“Nimebakiza kandarasi ya miezi minne na sijaongeza mkataba mwingine ila nikizungumza nao nitajua hatma yangu ndani ya Yanga.

“Kuhusu kupewa mkataba ama kutokupewa kwa sasa hilo siwezi kulizungumzia ila ninachojua mimi ni kwamba kazi yangu ni mchezaji na timu nyingi zinanihataji,” amesema.

SOMA NA HII  Ni nafasi kwa KMC kuomba kushiriki CECAFA