Home Habari za michezo NTIBAZOKINZA UHAKIKA….KRAMO BYE BYE SIMBA….MPANGO MZIMA UMEKAA HIVI…

NTIBAZOKINZA UHAKIKA….KRAMO BYE BYE SIMBA….MPANGO MZIMA UMEKAA HIVI…

Habari za Simba SC

Uongozi wa Simba umekaa kikao na kuazimia kuwaita mezani baadhi ya wachezaji wake wakiongozwa na washambuliaji Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ na Aubin Kramo ili kujadili mikataba yao.

Simba inataka kumwongezea Saido mkataba kabla haijafika Desemba ili kumdhibiti kuondoka kikosini hapo kwani mkataba wake wa awali (wa mwaka mmoja), aliousaini kwenye dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Geita Gold utamalizika Desemba.

Inafahamika kuwa  tayari Saido na Simba wameanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na kila pande imewasilisha matakwa yake na mchakato wa majadiliano unaendelea vizuri.

Wakati Saido akiwa mbioni kusaini mkataba mpya, hali iko tofauti kwa Kramo, ambaye mabosi wa Simba wanapiga hesabu za kuachana naye kwenye dilisha dogo, Januari, kutokana na kuandamwa na majeraha yanayomweka nje kwa muda mrefu.

Tangu alipojiunga na Wekundu wa Msimbazi, mwanzoni mwa msimu huu akitokea Asec Mimosas ya nchini kwao Ivoey Coast, kiungo huyo mshambuliaji hajacheza katika mechi yoyote ya kimashindano.

Kramo yuko nchini kwao akilikokwenda kwa matibabu, lakini imeelezwa viongozi wa Simba wapo tayari kufungua mazungumzo ya kuvunja mkataba ili kupata nafasi ya kusajili mchezaji mwingine na imepanga kushusha beki wa kimataifa.

SOMA NA HII  KISA 'KUILOGA' SIMBA...TFF WAISHUSHIA RUNGU LA ADHABU SINGIDA BIG STARS...