Home Habari za michezo MAXI AJA NA KIAPO HIKI LIGI KUU

MAXI AJA NA KIAPO HIKI LIGI KUU

yanga leo

Kiungo fundi wa boli, Maxi Nzengeli alisema anaendelea kuizoea ligi ya Tanzania akitaka kuvunja rekodi aliyoanza nayo ya kufunga na kuasisti kwa timu hiyo iliyomsajili kutoka AS Maniema ya DR Congo. Maxi anasema msimu uliopita katika ligi ya DR Congo hadi iliposimama alitengeneza asisti tatu na kufunga manne katika mechi nane Maniema.

“Ninapocheza kama kiungo jukumu langu kubwa ni kuzalisha pasi za mabao hili ndio nataka liwe linatangulia kwangu hizi mbili ni chache sana nataka kutoa pasi za mabao zaidi kuliko kufunga,” alisema Maxi na kufichua kuwa mzuka unaomfanya kufanya makubwa uwanjani ni umati wa mashabiki ambao wapo kila wanakokwenda.

“Hapa watu wanapenda sana mpira, kila unapokwenda unakutana na mashabiki wengi. Tena, sisi tunasafiri na ndege lakini wako mashabiki wengine wanasafiri kwa umbali mrefu kwa mabasi. Hawa ndio wanatufanya tuongeze juhudi uwanjani,” alisema.

SOMA NA HII  HAWA HAPA WACHEZAJI MAJERUHI WA SIMBA NA YANGA WALIOPONA...LIST KAMILI HII HAPA