Home Habari za michezo WAKATI WANIGERIA WAKIJA KWA GIA YA KUJIFANYA WANAHALI NGUMU…NABI KAWACHORA WEE..KISHA AKASEMA...

WAKATI WANIGERIA WAKIJA KWA GIA YA KUJIFANYA WANAHALI NGUMU…NABI KAWACHORA WEE..KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Yanga SC

Achana na taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii zilizodai kuwa Rivers United wanakabiliwa na ukata na hivyo wanaweza kuwasili nchini Jumamosi na kuondoka siku ya Jumatatu baada ya mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili.

Hizo ni mbinu tu wanajaribu kutumia ili ionekane kama wamekata tamaa na mchezo wa marudiano. Fahamu kwamba, Rivers United tayari wameshatua Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga SC.

Wananchi hawapaswi kuingia kwenye mtego wa kuaminishwa kuwa Rivers United wamekubali kipigo na hivyo wanakuja kukamilisha ratiba tu.

Jambo la uhakika ni kuwa mchezo wa Jumapili utakuwa mgumu, Yanga SC itapaswa kuchukulia kama ni mechi mpya pasipo kujali matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza.

Habari njema ni kuwa baada ya ushindi wa Nigeria wachezaji na benchi la ufundi walitarajia hicho walichokifanya Rivers United. Wamefeli kwani watarajie kukutana na Yanga SC yenye njaa ya kutinga nusu fainali.

Baada ya ushindi wa Nigeria, kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alibainisha kuwa bado hawajafuzu nusu fainali na kuwa ili kufanikisha hilo wanapaswa kushinda dhidi ya Rivers United baada ya mechi zote mbili.

Mechi iliyopigwa Nigeria wikiendi iliyopita na Yanga kushinda bao 2-0, ni kama dakika 90 za kwanza na hii itakayopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili ni dakika 90 za pili.

SOMA NA HII  WATANZANIA WAFELI MTIHANI WA UWAKALA FIFA...AFAULU MMOJA TU...