Home Habari za michezo WAKATI KIBU DENIS AKIMIMINIWA MAMILIONI TENA…WASAIDIZI WAPYA WA MBRAZILI SIMBA WATAJWA..

WAKATI KIBU DENIS AKIMIMINIWA MAMILIONI TENA…WASAIDIZI WAPYA WA MBRAZILI SIMBA WATAJWA..

Habari za Simba

Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis, ataendelea kuichezea timu hiyo, mara baada ya kufikia muafaka wa kuongeza mkataba wa miaka miwili.

Kibu alikuwa katika orodha ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu 2022/23, baada ya kujiunga na Simba msimu wa 2021/22 akitokea Mbeya City.

Kiungo huyo ndiye aliyefunga bao la pili katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata Simba dhidi ya Yanga katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara 2022/23.

Taarifa ambazo tumezipata, zinasema kwamba, sasa Kibu mkataba wake utamalizika Juni 2025 baada ya kuongeza miaka miwili.

Mtoa taarifa huyo alisema umuhimu na ubora wake Kibu ndiyo umewashawishi Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, kumuongezea mkataba huo.

“Hatuna mpango wa kumuachia mchezaji yeyote muhimu aliyekuwepo katika mipango ya timu kuelekea msimu ujao ambao tunakwenda kuandika historia katika michuano ya kimataifa.

“Tulichopanga ni kuwabakisha kwa kuwaboreshea mikataba yao ili tuendelea kubaki nao, huku tukiwaongeza wengine wapya watakaokuja kuifanya Simba imara.

“Kibu ni kati ya wachezaji ambao tuliowaongezea mikataba ya kuendelea kubaki Simba, kila mtu ameona kiwango cha mchezaji huyo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo la usajili, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alisema: “Hakuna mchezaji tegemeo atakayeondoka hapa Simba, kikubwa tutaendelea kuboresha mikataba ya wachezaji wetu.”

WASAIDIZI WA ROBERTINHO KUTANGAZWA

Aidha katika hatua nyingine, Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wanatarajia kutambulisha benchi zima la ufundi wiki hii baada ya kutangaza kuachana na Kocha wa Viungo, Kocha wa Magolikipa na Mchua Misuli.

Aakizungumzia suala hilo kupitia Simba APP, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahnmed Ally, amesema tayari wameshawapata watu mahiri kwa ajili ya kujaza nafasi ya benchi hilo la ufundi.

“Tumepata Kocha wa Viungo wa maana kweli kweli, tunataka wachezaji wetu wawe fiti haswa. Tumeshampata kocha wa magolikipa ambaye atawafanya makipa wetu wawe imara kwelikweli na vile vile mchua misuli, kifupi ndani ya wiki hii tutawatangaza,” alisema Ahmed.

Licha ya kuwa hakufafanua zaidi lakini inaaminika kuwa, watu hao wapya wanaoingia kwenye benchi la ufundi, watakuwa chini ya Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertihno’ na Kocha Msaidizi Juma Mgunda ‘Gadiola Mnene’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here