Home news AMBOKILE APEWA MWEZI MMOJA NKANA

AMBOKILE APEWA MWEZI MMOJA NKANA


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya soka ya Nkana inayoshiriki Ligi Zambia, Eliud Ambokile ameweka wazi kuwa Uongozi wa klabu yao umewapa mapumziko ya mwezi mmoja kabla ya kurejea tena kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

Ambokile alijiunga na Nkana mwezi Aprili mwaka huu kama mchezaji huru, akitokea ndani ya kikosi cha klabu ya TP Mazembe ya DR Congo baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya klabu hiyo.

Nkana hawakuwa na wakati mzuri kwenye msimu wa Ligi Kuu ya Zambia uliomalizika ambapo walimaliza katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi, na pointi zao 45 kwenye michezo 34.

Akizungumzia mipango yao, Ambokile amesema: “Baada ya kumaliza msimu huu, Uongozi wa klabu kwa kushirikiana na benchi la ufundi umetoa mapumziko ya mwezi mmoja kwa wachezaji wote.

“Baada ya mapumziko hayo tunatarajia kuanza maandalizi yetu ya kabla ya msimu ‘Pre-seasons’, ambayo tunatarajiwa kuanza mapema zaidi, ili kupata muda wa kutosha wa kurejesha makali ya kikosi chetu hasa baada ya changamoto ya kuwa na wakati mbaya msimu uliopita.”

SOMA NA HII  HAYA SASA NI SIMBA HAPO SEPTEMBER 14