Home Habari za michezo FT: SIMBA 1-0 JAMHURI…..BALEKE KAMA YUPO HAYUPO HIVI…KIUNGO MPYA AKIWASHA ..ILA MHH..

FT: SIMBA 1-0 JAMHURI…..BALEKE KAMA YUPO HAYUPO HIVI…KIUNGO MPYA AKIWASHA ..ILA MHH..

FT:Simba 1-0 Jamhuri

Simba imeendelea kuweka salama malengo yao ya kuchukua taji la pili msimu huu ikitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba kwa bao 1-0.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Simba kuifuata Singida Fountain Gate ambao mapema jioni ilitangulia nusu fainali baada ya kuichapa Azam FC kwa mabao 2-1.

Simba haikuwa na dakika 90 rahisi mbele ya Jamhuri kama ambavyo ilikuwa ikidhaniwa kwani vijana hao wa Pemba walikuja na akili tofauti na mbinu na kuwabana vizuri wekundu hao kwa muda mwingi wa mchezo huo.

Jamhuri waliwabana Simba kwa kuwa bora katika njia za kupitisha mipira ya kutengeneza mashambulizi ya wekundu hao na kuwaweka kwenye presha kubwa wapinzani wao.

Simba ingeweza kutengeneza ushindi mzuri pengine zaidi kama washambuliaji wake Jean Baleke na Luis Miquissone wangetulia kutumia nafasi hasa kupitia krosi za mabeki wao wa pembeni wakiongozwa na Shomari Kapombe

Shambulizi kali la Jamhuri lilifanyika dakika ya 83 walipofika vizuri na kupiga shuti kali ambalo hata hivyo lilipanguliwa na kipa Ayoiub Lakred kisha kuudaka tena.

Muda mrefu ukuta wa Simba ulikuwa kwenye utulivu mkubwa kutokana na kukosa changamoto kutoka kwa washambuliaji wa Jamhuri ambao walidhibitika kirahisi.

Baleke kosa moja tu

Ukuta wa Jamhuri ulifanya kosa moja tu lililowagharimu kwa kumruhusu mshambuliaji Jean Baleke kuruka juu bila kusumbuliwa na kufunga bao hilo pekee lililoamua mchezo huo akitumia krosi ya Miquissone dakika ya 45+2.

Ngoma na tuzo za mchezaji Bora

Kiungo wa Simba Fabrice Ngoma ni kama ameziteka tuzo za mchezaji bora za timu hiyo akichukua tuzo ya pili kwenye mechi za Singida Fountain Gate na leo dhidi ya Jamhuri.

Singida vs Simba ni kisasi

Simba kwenda kukutana na Singida ni kama mechi ya kisasi kwani timu hizo zilikutana hatua ya makundi na Singida kukubali kipigo cha mabao 2-0.

SOMA NA HII  CHAMA,MUSONDA WAREJEA ZAMBIA..... ISHU IKO HIVI