Home Uncategorized KIPA MPYA YANGA AIPA UBINGWA MAPEMA

KIPA MPYA YANGA AIPA UBINGWA MAPEMA


MLINDA Mlango mpya wa Yanga, Metacha Mnata amesema kuwa hana hofu na changamoto mpya ambazo atazipata ndani ya kikosi chake hicho.

Mnata amejiunga na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea klabu ya Mbao FC.

“Najua kazi ni kubwa msimu mpya na nipo ndani ya Yanga kwa kuwa kazi yangu ni mpira, sina mashaka na kipaji changu nitapambana kufanya vema na malengo ni kuona tunabeba makombe.

“Changamoto mpya ni kitu cha kawaida kwa mchezaji hivyo ni suala la muda tu kusubiri nini kitatokea msimu ujao,” amesema.

SOMA NA HII  JINGINE LAIBUKA JUU YA MKATABA WA GADIEL YANGA, MILIONI 40 ZATAJWA