Home Uncategorized JINGINE LAIBUKA JUU YA MKATABA WA GADIEL YANGA, MILIONI 40 ZATAJWA

JINGINE LAIBUKA JUU YA MKATABA WA GADIEL YANGA, MILIONI 40 ZATAJWA


YANGA wamejiwekea msimamo kwamba wachezaji wote wazawa kila mmoja mkwanja wake wa usajili usizidi Sh.Mil 30 lakini kuna baadhi wanaweza kuwafi kiria kidoogo.

Gadiel Michael ni mmoja wao. Sasa wakubwa wakamuendea hewani wakamwambia ; “njoo umwage wino kuna mil 40 hapa.”

Gadiel akawaambia “niongezeeni kidogo kwavile mara ya kwanza mlinipa Mil 30 wakubwa” Yanga wakamwambia hamna noma njoo fasta tuyajenge, Gadiel akawasha gari kuwafuata viongozi wakati yuko njiani akamtumia meseji wakala wake kwamba; “Mimi ndio naenda kuwasikilizia jamaa.”

Meneja akamuendea hewani fasta akamwambia ; “Wee…usiende rudi, ukiwapa nafasi ya uso kwa uso watakushinda.”

Mchezaji akageukia njiani Yanga wakasubiri weee… wakaishia kumsainisha Papy Tshishimbi. Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra imezipata ni kwamba mpaka jana Gadiel alikuwa anakomaa na Yanga akitaka wampe Sh.60Mil kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo wa zamani wa Azam anatajwa pia kuwindwa na Simba na mashabiki wametengeneza jezi ya mitandaoni wakiwarusha roho Yanga. Gadiel ni kati ya wachezaji 15 ambao mikataba yao imemalizika na Zahera amesisitiza kwamba wanaweza kuondoka tu kama akiamua vinginevyo kwavile ana wachezaji kibao.

SOMA NA HII  MITAMBO HII NANE YA KAZI YAINGIA ANGA ZA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here