Home Yanga SC YANGA KUMALIZANA NA MGHANA HUYU

YANGA KUMALIZANA NA MGHANA HUYU


 EDEM Mortotsi nyota wa zamani wa Klabu ya FC Edmontok yupo kwenye hesabu za mwisho za kumalizana na vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 msimu wa 2020/21.

Mortosi mwenye umri wa miaka 27 tayari yupo Dar es Salaam tangu jana kwa ajili kukamilisha dili hilo kabla ya kusaini kandarasi yake na anatajwa kuwa atakuwa kwenye benchi la ufundi. 

Mortotsi alizaliwa nchini Ghana lakini alikulia Edmonton nchini Canada. Alichezea Klabu ya FC Edmonton kwa miaka saba kuanzia Aprili 2013 hadi Desemba 2020.

Msimu wa 2020 hakuwa ndani ya uwanja kuonyesha makeke yake kutokana na majeraha na aliletwa duniani Aprili 16,1993.

SOMA NA HII  KWA KAULI HII YA KITASA KIPYA CHA JANGWANI....MASHABIKI YANGA MSIPOANGALI MTAUMWA KISUKARI...