Home Taifa Stars KILA LA KHERI TAIFA STARS LEO PAMBANENI KUFANYA KWELI

KILA LA KHERI TAIFA STARS LEO PAMBANENI KUFANYA KWELI

LEO ni leo asemaye kesho huwa anatajwa kuwa ni muongo. Huu ni msemo ambao wahenga walitufundisha zama zile wakati wa matatizo makubwa ambayo tulipitia ama katika kusaka ushindi wa namna yoyote ile.

Hatimaye ile siku ambayo inasubiriwa kwa shauku kubwa na wapenda soka Tanzania imewadia nayo ni leo. Hakuna siku nyingine tena zaidi ya leo kuwa ni siku ya furaha na pia inaweza kuwa ya huzuni pia.

Ninasema hivyo kwa sababu kazi iliyopo mbele ya timu yetu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni leo kupambana kufikia ndoto zile ambazo zilikuwa zinaotwa na Watanzania wengi kwa muda mrefu.

Ile ndoto ya kutinga hatua ya robo fainali ni ndoto ambayo inapaswa itimie leo kwa Stars kushinda kwenye mchezo wake dhidi ya Guinea hakuna habari nyingine.

Ukweli upo wazi kwa kila Mtanzania kupenda kuona timu ya Tanzania inafanya vizuri.Na inawezekana ikiwa kila mmoja akatimiza wajibu wake ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

Kwa kundi D ambalo linaongozwa na Guinea wenye pointi nne sawa na Namibia wenye pointi nne hapo ina maana kwamba ikiwa timu itapata ushindi kwenye mchezo wa leo inapenya jumla hatua ya robo fainali.

Nina amini kwamba wakati huu wa haya mashindano ya Chan wapo ambao watafungua ukurasa wao mpya wa kutoka katika ulimwengu wa mpira. Njia ni moja tu kwa wachezaji kucheza kwa juhudi na kusaka matokeo bila kukata tamaa.

Kinachotakiwa leo kwa wachezaji wote ndani ya uwanja ni kupambana bila kukata tamaa na kusaka ushindi ndani ya dakika 90 ili kukata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali inawezekana.

Ni muda wa kazi ndani ya uwanja kwa kila mmoja hizi dakika 90 ambazo mnazo leo zimeshika funguo ya furaha kwa mashabiki na funguo ya mafanikio kwa timu ya Taifa ya Tanzania.

Kuna suala la timu kupanda viwango kwa Tanzania kiujumla hili ni jambo la msingi na hapa ndipo ambapo ramani ya mafanikio kwa soka la Tanzania inachorwa leo.

Hakuna ambacho kwa sasa kinasubiriwa na mashabiki pamoja na taifa kiujumla zaidi ya kushangilia ushindi wa leo hivyo wachezaji hili ni deni kwenu.

Mkiingia uwanjani mnapaswa kuwa watulivu na kucheza kwa nidhamu kubwa kwa kuwa ikiwa mtaingia kwa presha ni rahisi kushindwa kufikia yale ambayo mnayatarajia kuyafanya.

Yale ambayo mmepewa na benchi la ufundi ni muhimu kuyafanya ndani ya uwanja na pia ni lazima kila mmoja aongeze juhudi binafsi ndani ya uwanja. Kazi ni moja kupambana kusaka ushindi.

Ni wazi kwamba kila mchezaji anapenda kufanya vizuri lakini asisahau kwamba inacheza timu wala hachezi mchezaji mmoja hivyo ni lazima wachezaji mpambane huku mkishirikiana.

SOMA NA HII  HATMA YA SAMATTA, MSUVA NA DISMAS STARS KUJULIKANA

Benchi la ufundi nalo pia kwenye upangaji wa kikosi lipange kikosi cha ushindi ninaona kwamba ikiwa wataweza kufanya mabadiliko kwenye kikosi pia tutarajie mabadiliko kwenye matokeo.

Duniani kote mwalimu huwa anakuwa na kikosi cha ushindi na kuna kikosi ambacho tayari kimeshazoeana kuleta ushindi hapo akili inahitajika katika kikosi cha leo na wale ambao watapangwa kazi yao iwe moja kupambana kusaka matokeo ndani ya uwanja.

Wachezaji 11 ni alama tosha ya ushindi leo na umoja wa kila mchezaji ni nguvu ya ushindi ukichanganya na dua za mashabiki pamoja na wachezaji basi kazi inakuwa imemalizika.

Ukweli usiofichika ni kwamba namna ambavyo tunahitaji kushinda hata wapinzani wetu pia Guinea wanahitaji kushinda. Hapo kinachohitajika ni kitu kimoja juhudi isiyo ya kawaida kwa wachezaji.

Kikubwa ambacho wachezaji wanapaswa wakifanye ni kujitambua na kubeba nguvu ya kujiamini kwamba wanaweza kupata matokeo uwanjani kwa kupambana bila kuchoka.

Jambo la msingi kwa sasa ni kila mchezaji kujua kwamba anatambua anakutana na ugumu mkubwa ila furaha yake iwe kwenye kusaka ushindi ndani ya uwanja bila kukata tamaa.

Imani yangu ni kwamba kila kitu kinawezekana na ushinid upo kwenye miguu yenu hivyo fanyeni kweli pambaneni bila kuchoka kusaka ushindi tunawaamini wapambanaji wetu.

Kama wachezaji mtaamua kujituma uwanjani pasipo kumtegemea mchezaji mmoja maana yake ni kwamba mtapata matokeo mazuri ambayo mnayafikiria.

Ila kama kila mmoja atakuwa anajiona yeye ni bora kuliko mwingine hapo ndipo tatizo linapoanzia hasa kwa kufanya ushindani na ule ubora kupotea.

Leo kila mmoja ni bora na kila mmoja ni mshindi. Imani ni kwamba anayeweza kutetea taifa letu leo ndani ya uwanja inawezekana na kila mchezaji anaweza kuleta ushindi kwa ajili ya taifa.

Kila mmoja akubali kujitoa kwa ajili ya timu na afanye kazi kwa juhudi akiwa uwanjani.Furaha ya wachezaji ni ushindi na furaha ya Watanzania ni ushindi, kila la kheri.

Tunaamini kwamba tunaweza kufanya mapinduzi katika soka letu kwa kupata matokeo na kuushangaza ulimwengu kwa sababu kila mmoja ni mshindi kwa sasa.

Watanzania tusisahau pia kuwaombea dua hawa wanajeshi wetu ambao watakuwa kazini kusaka ushindi. Kila mmoja ana kazi ya kutimiza majukumu yake.

Hivyo ni muhimu wachezaji wetu kutambua kwamba kazi yao leo iweze kutimia lazima wapambane kushinda na itawafungulia pia milango ya kupata timu nyingine nje ya Bongo.

Chan inafuatiliwa na wengi hivyo kwa wale ambao wanafanya vizuri kazi inakuwa moja kwa mawakala kuweza kuzungumza nao na kufungua ukurasa wa kufanya nao biashara.