Home Simba SC MASTAA WATATU WENGINE WAPYA WANAOFUNGA USAJILI SIMBA HAWA HAPA

MASTAA WATATU WENGINE WAPYA WANAOFUNGA USAJILI SIMBA HAWA HAPA

 WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya mabingwa Afrika, Simba watafunga usajili wa Shirikisho la soka Afrika (Caf), kwa kushusha mashine za maana si chini ya wachezaji watatu.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinaeleza tayari wachezaji hao watatu kati yao wawili wameshafika nchini na muda wowote watatambukishwa na kuanza kazi ya kuitumikia timu hiyo.

Mwanaspoti imepata taarifa kuwa nyota hao ni  Mkongomani mmoja, Doxa Gikanjia ambaye tayari amesainishwa mkataba wa miezi sita na sasa yuko katika majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo, inayoshiriki mashindano ya Chan, huko nchini Cameroon.

Kiongozi mmoja wa Simba, mwenye maamuzi ndani ya timu hiyo alisema tayari wamemaliza usajili wa Gikanji  na sasa wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Mzimbabwe mmoja kati ya wawili  ambao tayari majina yao yapo mezani.

“Wazimbabwe hao ni Peter Muduwa na Talent Chamboko ambao wote wanacheza nafasi ya beki wa kati na tunaweza kumalizana nao wakati wowote kuanzia sasa. ,” amesema

Kiongozi huyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake.

Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, alisema wanafanya usajili katika kipindi hiki ili kuboresha timu hiyo  hasa wakiangalia zaidi  mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Bodi ya Wakurugenzi iliyokuwa chini ya Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ inafanya kazi ya kuboresha kikosi chetu ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya klabu.

“Malengo ya timu ni kufika nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na ili tufanikiwe lengo hilo ni lazima tujiandae  ndio maana tumefanya usajili wa kocha bora pamoja na kuleta wachezaji hawa wa maana,”  amesema Kaduguda.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAONA HAWAKO 'SIRIAZI'...SAID BAHANUZI AAMUA KUWACHANA WACHEZAJI SIMBA...AMTAJA BOCCO..