Home Habari za michezo KAMA HUNA DEGREE YA CHUO KIKUU …SAHAU UBOSI NDANI YA SIMBA…

KAMA HUNA DEGREE YA CHUO KIKUU …SAHAU UBOSI NDANI YA SIMBA…

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba, Boniface Lyamwike leo amewatangazia Wanachama wa Simba, Wapenzi na Mashabiki kwamba tarehe ya uchaguzi wa Simba ni 29 January 2023 na kwamba kigezo cha yeyote anaeutaka Uenyekiti wa SIMBA lazima awe na degree ya Chuo Kikuu.

“Mtu yeyote ambaye anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ni lazima awe na angalau shahada ya Chuo Kikuu na lazima awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha Club ndani na nje ya nchi.

“Anayegombea nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi lazima awe amefika kidato cha nne na cheti za kuhitimu, kigezo kingine awe mzoefu wa angalau miaka mitatu ya Uongozi wa mpira wa miguu.

“Kingine asiwe amepatikana kamwe ya hatia ya kosa ya jinai, lakini pia angalau awe na miaka 25 na si zaidi ya miaka 64, lakini pia asiwe Mmiliki, Mwanahisa au Kiongozi wa Timu nyingine ya mpira wa miguu,” amesema Boniface Lyamwike.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTINGA FAINAL YA FA...TUCHEL AWAVURUMISHIA KOMBORA LA MANENO YA KEJELI LIVERPOOL...