Home Uncategorized PACHA WA MWAMNYETO, AME, PICHA ZIMA KUIBUKIA SIMBA LIMECHEZWA HIVI

PACHA WA MWAMNYETO, AME, PICHA ZIMA KUIBUKIA SIMBA LIMECHEZWA HIVI


IBRAHIM Ame aliyekuwa pacha wa Bakari Mwamnyeto ndani ya Coastal Union inayonolewa na Juma Mgunda inaelezwa kuwa amemalizana na mabosi wa Simba kwa dili la miaka miwili.

Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck ilikuwa kwenye rada za kumnasa Mwamnyeto kwa muda mrefu na ilimvutia waya kuja Dar es Salaam kabla ya nyota huyo kupokelewa na watu wa Yanga.

Mtoa taarifa anaeleza kuwa ilikuwa ngumu kwa beki huyo aliyetupia bao moja ndani ya ligi kukubali kusaini Yanga kwa kuwa alikuwa anajua kwamba anahitajika ndani ya Simba ila mabosi wa Yanga walipomshawishi akawa hana chaguo.


“Picha linaendelea baada ya mabosi wa Simba kugundua kuwa wamepigwa bao na watani zao wa jadi Yanga nao wakaingia kwenye rada za kuinasa saini ya Ame ambaye naye ilibidi atambulishwe ndani ya Yanga, usiku wa Jumanne, Agosti 4.

” Akiwa Dar, Ame baada ya kutumiwa nauli na watu wa Yanga alikutana na mabosi wengine wa Simba ambao walimpeleka ofisini maeneo ya Posta na kumpa mkataba wa miaka miwili, hakuwa na chaguo zaidi ya kumpigia simu meneja wake na kumwambia kuwa haelewi mambo yanakwendaje.

“Meneja naye alipokuja maeneo ya Posta akashawishiwa na watu wa Simba na kukubali mteja wake asaini kisha akawapigia simu watu wa Yanga kuwa dili la Ame mambo yameshindikana,” ilieleza taarifa hiyo.

Ame amesema:”Nimekuja Dar nipo na mazungumzo na watu wa Simba mambo yakikamilika kila kitu kitakuwa wazi.”
SOMA NA HII  BEKI YANGA AMPA KICHEKO KOCHA POLISI TANZANIA