Home Uncategorized AZAM FC YAMALIZANA NA KIPA ALIYEKUWA AKIKIPIGA KENYA

AZAM FC YAMALIZANA NA KIPA ALIYEKUWA AKIKIPIGA KENYA

DAVID Kissu kipa aliyekuwa akikipiga Gor Mahia ya Kenya leo amefuzu vipimo vya afya kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Azam FC.

Kissu aliibukia Gor Mahia akitokea Klabu ya Singida United, amewahi kuitumikia Njombe Mji pia alikokuwa akikipiga na Ditram Nchimbi ambaye naye alikipiga Azam FC kabla ya kuibukia Mwadui FC  kisha Polisi Tanzania na sasa yupo Yanga.

Pia kipa huyo alikuwa ana namba ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivi karibuni kabla ya janga la Virusi vya Corona kuvurugavuruga mambo.

Inaelezwa kuwa amesaini dili la miaka miwili ndani ya Azam FC kuwa  mbadala wa Razack Abarola ambaye mkataba wake umeisha na kwa sasa yupo zake Ghana.

SOMA NA HII  AKILI ZA HARUNA NIYONZIMA NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA