Home news SAA CHACHE KABLA YA MECHI KUANZA…HIVI NDIVYO SAKHO, BANDA WANAVYOMPA JEURI PABLO…

SAA CHACHE KABLA YA MECHI KUANZA…HIVI NDIVYO SAKHO, BANDA WANAVYOMPA JEURI PABLO…

 


KUREJEA kwa Pape Ousmane Sakho ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya ASEC Mimosas na kuimarika kwa kiwango cha winga Peter Banda, kumempa kiburi Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco kufanya vizuri katika mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Union Sportive Gendarmerie Nationale ya nchini Niger.

Simba leo Jumapili wanatarajiwa kumenyana na Union Sportive Gendarmerie Nationale katika mchezo wa pili wa Kundi D ndani ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa kwenye Dimba la Général Seyni Kountché lililopo Niamey, Niger.

Katika hatua ya makundi, Simba imeanza vizuri ikishinda mchezo wa kwanza nyumbani kwa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Kwa upande wa wapinzani wao wa leo, walipoteza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya RS Berkane ya nchini Morocco kwa kufungwa mabao 5-3.

Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo aliweka wazi kuwa, Sakho tayari yupo fiti baada ya kukosekana katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting, huku akifurahishwa na baadhi ya wachezaji wake ambao viwango vyao vimezidi kuimarika akiwemo Banda na Israel Patrick Mwenda.

“Sakho yupo fiti kwa sasa, tuliona ni vema kumpumzisha katika mchezo dhidi ya Ruvu, lakini yupo vizuri kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Union Sportive Gerndamarie.

“Wachezaji wapo tayari kwa mechi na habari njema ni kwamba wachezaji wengi wameonekana kuimarika tofauti na awali. Peter Banda na Israel Mwenda ni mfano katika hili, wengine pia wanafanya vizuri, naamini watakuwa msaada kwetu kwa ajili ya kufanya vizuri katika mchezo huu,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AWATULIZA WANASIMBA AFUNGUKA HAYA