Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO….SIMBA WAMVIKA ‘MABOMU MAALUMU’ KIBU DENIS…UKWELI UKO HIVI…

KUELEKEA MECHI YA KESHO….SIMBA WAMVIKA ‘MABOMU MAALUMU’ KIBU DENIS…UKWELI UKO HIVI…

Habari za Simba SC

Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis, amepewa jukumu zito la kuhakikisha anatumia aina yake uchezaji ya spidi kuivuruga safu ya ulinzi ya Al Ahly.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kesho Ijumaa (Oktoba 20) saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam katika mchezo wa ufunguzi wa African Football League (AFL).

Kuelekea mchezo huo, Simba SC imepanga kupata ushindi mkubwa nyumbani kabla ya kwenda kurudiana Oktoba 24, mwaka huu Cairo, Misri.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema amewaona wapinzani wao Al Ahly kupitia video za michezo yao iliyopita, hivyo hana hofu.

Robertinho amesema Al Ahly wanacheza soka la taratibu wakati wakianzisha mashambulizi yao, ni hatari kuwaacha wakimiliki mpira muda mrefu, hivyo amepanga kuwatumia wachezaji wenye kasi kuwadhibiti wapinzani wa kwa kuanzia golini kwao.

Amemtaja kiungo wake Kibu ndiye atakayempa kazi hiyo ya kuwapora mipira wapinzani na kuanzisha mashambulizi kwa spidi kwa lengo la kuwachosha ili wapate matokeo mazuri.

“Aina ya ucheza ya Al Ahly sio ya kasi na wamekuwa wakikutana na wakati ngumu wanapocheza na timu zenye kasi mfano dhidi ya Wydad Casablanca na Mamelodi Soundown.”

“Wachezaji wake wengi wamekuwa wakicheza taratibu, lakini kwa uhakika zaidi, hivyo mara nyingi hawapendi kukutana na timu ambayo ina mawinga wanaokimbia sana.

“Kuelekea mchezo huu, nimempa majukumu mazito Kibu ya kuhakikisha anaisumbua safu ya ulinzi ya Al Ahly akitumia nguvu na kasi kushambulia goli la wapinzani wetu, tayari nimempa maelekezo na majukumu anayotakiwa kuyafanya,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOSHUKA DIMBANI DHIDI YA MTIBWA SUGAR