Home news HUYU HAPA BEKI WA WANIGER WANAOCHEZA NA SIMBA AMBAYE ALIJIFUNGA GOLI MBILI...

HUYU HAPA BEKI WA WANIGER WANAOCHEZA NA SIMBA AMBAYE ALIJIFUNGA GOLI MBILI MAKUSUDI KISA KUBETI


SIMBA imetua nchini Niger jana tayari kwa mechi ya leo Jumapili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USGN FC, lakini wanakutana na beki mwenye rekodi ya ajabu.

Kwenye kikosi cha kwanza cha USGN pale kati kuna beki Mghana Hashmin Musah ambaye mwaka jana aliwaacha watu hoi kwenye Ligi Kuu ya Ghana akiichezea Inter Allies baada ya kujifunga mabao mawili makusudi kwa kile alichodai kwamba wenzake walikula mchongo wa kubeti mechi iishe kwa wao kupoteza mabao 5-1.

Beki huyo alikiri kufanya tukio hilo kwenye mechi iliyoisha kwa mabao 7-1 dhidi ya Ashanti Gold na kuadhibiwa ingawa baadaye kesi iliisha kiaina baada ya mchezaji huyo kuibukia Niger. Lakini baada matokeo ya juzi ya USGN kupigwa mabao 5-3 ugenini dhidi ya Berkane sakata lake likaibuka baada ya wadau wengi kushtukia kwamba anaichezea timu hiyo huku baadhi wakidai ndiyo michongo yake. Ingawa hakukuwa na kiashiria cha moja kwa moja kwenye mechi hiyo kwamba alijifunga japo kichambuzi alipwaya.

Kwenye mechi hiyo ya msimu uliopita aliyofunga mabao mawili akiingia dakika 12 kabla ya mechi kumalizika na kukiri baadaye alifanya hivyo makusudi ili kuharibu dili ya wenzie ambao walikuwa wamebeti.

“Nilifanya vile makusudi kwa vile kabla ya mchezo nilisikia pale hoteli wakisema matokeo yawe 5-1, ndio maana nilivyoingia nikafunga ili kuharibu,” alisema beki huyo bila aibu ingawa wengi walishinikiza afungiwe ili kufuta aibu hiyo kwenye Ligi ya Ghana. Matokeo ya Berkane yameibua ishu ya mchezaji huyo huku baadhi ya wachambuzi wa Ghana wakihoji alisafishwaje kwenye kashfa yake na kupewa kibali cha kucheza nje ya nchi.

Baadhi walidai kwamba alikuwa amezuiwa kucheza soka kwa muda na timu yake ilishuka daraja msimu uliopita. Simba inatua Niger jioni hii kuwakabili USGN na hawatakuwa na muda wa kufanya mazoezi ya mwisho kutokana na kushindwa kufika kwa wakati.

Lakini, Kocha Pablo Franco amesisitiza kwamba watakomaa kwenye mazingira watakayokumbana nayo kwani hata kwenye Ligi Kuu walikuwa wamebanwa na ratiba ingawa amekiri kwamba hawatarajii ushindi kwenye mechi mbili za ugenini kutokana na uhalisia wa michuano hiyo ya Afrika ila watapambana.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUANZA KUTUPIA SIMBA SC...NTIBAZONKIZA AWACHANA WANAYANGA...

Simba kwenye mechi ya mwisho ya Kombe la FA walishinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Masau Bwire.