Home Uncategorized BINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU WA 2019/20 ATAPATIKANA KWA MTINDO HUU

BINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU WA 2019/20 ATAPATIKANA KWA MTINDO HUU


MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Almas Kasongo amesema kuwa hatma ya bingwa wa ligi itaamuliwa uwanjani na si vinginevyo.

Kwa sasa ligi imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.

Wakati ligi ikisimama Simba ilikuwa inaongoza ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28.

Kasongo amesema kuwa wanaamini hali itakuwa shwari baada ya muda na bingwa wa ligi atapatikana ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  LIGI KUU BARA: MBAO 0-0 SIMBA