Home Habari za michezo KIBADENI ASEMA HAYA KWA ANAYETAKA KUPIGA HAT TRICK SIMBA, YANGA

KIBADENI ASEMA HAYA KWA ANAYETAKA KUPIGA HAT TRICK SIMBA, YANGA

Habari za Michezo

Abdallah Athumani Seif ‘King Abdallah Kibadeni Mputa’ nyota wa zamani wa Simba ndiye mchezaji pekee aliyefunga ‘hat trick’ katika Kariakoo Derby, akifanya hivyo katika pambano la kihistoria lililopigwa Julai 19, 1977.

Katika pambano hilo lililokuwa la 11 tangu Simba na Yanga kuanza kukutana katika Ligi iliyoasisiwa mwaka 1965, Kibadeni alifunga mabao hayo matatu wakati Simba ikiwafumua watani wao kwa mabao 6-0.

Kibadeni alifunga mabao yake katika dakika ya 10, 42 na 89, huku mengine yakiwekwa kimiani na Jumanne Hassan ‘Masimenti’ dk. 60 na 73 na beki wa Yanga, Selemani Sanga alijifunga katika dakika ya 20 ya mchezo huo.

Imefika miaka 46 sasa hakuna nyota yeyote wa klabu hizo aliyeweza kuvunja rekodi hiyo ya Kibadeni, licha ya Simba na Yanga kusajili kila msimu mastaa wa ndani na nje ya Tanzania.

King Kibaden amesema iwapo kuna mchezaji anatamani kufunga hattrick kwenye mechi ya Simba na Yanga, basi aisisite ajitokeze na aende kwake amuomba atamruhusu, vinginevyo rekodi yake hiyo ahiwezi kuvunjwa na mtu yoyote mpaka atakapoondoka duniani.

“Nimeshasema mara nyingi, ile kazi mimi sikuipata hivi hivi, anayetaka kufika kwenye rkodi yangu si aje kuniomba mimi? Akiomba kwenye klabu haiwezi kumsaidia, aje kuniomba mimi nimuachie kwa sababu mimi. Nimefunga na rekodi itaendelea kuwepo mpaka Mungu aniondoe ndiyo yaje masuala mengine.

“Nikiwa hai hatoei mtu wa kufunga hattrick kwenye Simba vs Yanga ndiyo maana nasema aje kuniomba, tena aseme Kibadeni naomba uridhie nifanye hiyo kazi kwani nani hataki sifa? Mimi nataka sifa, mnavyosema kwamba rekodi ya miaka 45, mimi nataka rekodi ya miaka 100.

“Kufungana watafungana lakini mtu mmoja kufunga bao 3 kwenye Simba na Yanga hiyo mpaka mimi labda ninyongwe, nasema aje aniombe akiwa yanga au Simba aje, kama hawataki tuendelee na rekodi yangu iliyopo,” amesema Kibadeni.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO YANGA NA RAIS SAMIA WALIVYOAMSHWA SHANGWE LA 'KUFA MTU' JANA MALAWI...