Home Habari za michezo FT: USM 0-1 YANGA….WAMEKUFA KIBABE…NABI AMWAGA CHOZI HADHARANI…MAYELE , DIARRA WAWEKA HISTORIA…

FT: USM 0-1 YANGA….WAMEKUFA KIBABE…NABI AMWAGA CHOZI HADHARANI…MAYELE , DIARRA WAWEKA HISTORIA…

USM vs Yanga

Wamekufa Kibabe., ndivyo unavyoweza kusema baada ya Yanga SC kushindwa kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni dakika chache baada ya mchezo wa mkondo wa pili wa fainal kumalizika hivi punde licha ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya USM Alger.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa aina yake, Yanga wameshindwa kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki baada ya matokeo waliyoyapata leo kuwafanya kuwa sawa kwa magoli 2-2 huku wenyeji wakinufaika kwa goli la ugenini.

USM Alger walifanikiwa kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza Jijini Dar es Salaam hivyo leo walihitaji sare au wasifungwe zaidi ya goli 1 ili kutwaa ubingwa huo ambao nao pia ni mara yao ya kwanza.

Yanga walianza kwa kasi kulishambulia lango la wapinzani wao, ambapo katika dakika za mwanzoni kipindi cha kwanza, walifanikiwa kupata penalti baada ya Musonda kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.

Ni Shabani Djuma ambaye alifanikiwa kuiweka Yanga mbele na goli la pekee kwa mchezo huo, kwa kuukwamisha mpira kwenye nyavu.

Yanga waliendelea kulisakama lango la USMA lakini uimara wa mabeki wa timu hiyo uliwafanya Mayele na Musonda kushindwa kuweka mpira kambani.

Aidha, Almanusura dakika 30 Mayele angeweza kuipatia Yanga goli la Pili lakini mabeki wa USMA walimzonga na kushindwa kufanikisha mpango huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, ambapo safari hii ni USMA walipata penati, mara baada ya Ibrahim Bacca kumfanyia madhambi Straika wa USMA.

Hata hivyo, Penati hiyo iliyopigwa na Nahodha wa USMA iliokolewa vyema na Mlinda mlango wa Yanga Djigui Diarra ambaye pia ameibuka kama mchezaji bora wa mechi hiyo.

Kwa matokeo haya, Yanga wamepata medali ya Shaba, pamoja na zawadi ya fedha kiasi cha zaidi ya Bilioni 2 za kitanzania, huku TFF nao wakilamba Milioni 100 kwa Yanga kufikia hatua hiyo.

Aidha, Yanga wameongeza alama 4 kwenye alama za ujumla kwa Tanzania kwenye mashindano ya CAF, huku Mayele yeye akiibuka mfungaji bora wa mashindano hayo akiwa na magoli 7.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Yanga Nabi, alionekana akimwaga machozi hadharani mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa ikiwa ni ishara ya kuumia kwa kushindwa kutimiza ndoto ya kuwa kocha wa kwanza kuleta kombe la CAF Tanzania.

SOMA NA HII  SIMBA WAAMUUA KUKISUKA UPYA KIKOSI CHAKE...WATENGA MAMILION KWA BEKI TU...IBENGE ATIA NENO....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here