Home news SABABU YA WAAMUZI SIMBA VS YANGA KURUDIWA HII HAPA

SABABU YA WAAMUZI SIMBA VS YANGA KURUDIWA HII HAPA


KAMATI ya Waamuzi wa Ligi Kuu Bara, imeweka wazi sababu za kurudia majina ya waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo wa Kariakoo dabi uliopigwa juzi Jumamosi  kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Orodha hiyo ambayo iliwekwa wazi na Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB), ilionyesha kuwa waamuzi waliochezesha mchezo wa jana ni walewale ambao hapo awali walipangwa kuchezesha mchezo wa Mei 8, mwaka huu kabla ya mchezo huo kuahirishwa.

Akizungumzia kutokuwepo kwa mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Soud Abdi Mohamed, amesema: “Kama Kamati tuliona hakukuwa na haja ya kubadilisha waamuzi ambao walipangwa kuchezesha mchezo uliopangwa kuchezwa Mei 8, mwaka huu kabla ya kuahirishwa kutokana na sababu zilizokuwa zimejitokeza.

“Hii ni kwa sababu tayari maandalizi ya mchezo ule yalikuwa tayari yamefanyika, na kukamilika, na tuliamini kuwa waamuzi waliokuwa wamepangwa walikuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutimiza majukumu yao kwenye mchezo wa Jumamosi.”

Orodha kamili ya maofisa waliosimamia mchezo Na. 208 wa Ligi Kuu ya Vodacom (Simba SC vs Young African SC) juzi Julai 3, 2021 ni kama ifuatavyo;

Kamisaa wa mchezo – Hosseah Lugano (Lindi)

Mwamuzi wa kati – Emmanuel Mwandembwa (Arusha)

Mwamuzi msaidizi namba moja – Frank Komba (Dar)

Mwamuzi msaidizi namba mbili – Hamdan Saidi (Mtwara)

Mwamuzi wa akiba – Ramadhani Kayoko (Dar)

Mtathmini wa mwamuzi – Soudy Abdi (Arusha)

Afisa mhusika – Jacquiline Kwamwamu (Dar)

SOMA NA HII  STARS YAIBUKA NA USHINDI MBELE YA MADAGASCAR