Home news STARS YAIBUKA NA USHINDI MBELE YA MADAGASCAR

STARS YAIBUKA NA USHINDI MBELE YA MADAGASCAR

 TIMU ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim

Poulsen leo Septemba 7 imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Madagascar. 

Ni katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Uwanja wa Mkapa na hakukuwa na mashabiki kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Mabao ya Stars yalifungwa na Erasto Nyoni kwa mkwaju wa penalti Novatus Dismas na yote yalirudishwa kipindi cha kwanza na ubao ulisoma Tanzania 2-2 Madagascar. 

Kipindi cha pili baada ya mapumziko vijana wa Stars waliweza kujipanga na kusaka ushindi kwa juhudi. 

Pasi ya upendo kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta ilikutana na miguu ya Feisal Salum ambaye alipachika bao la ushindi. 

SOMA NA HII  MORRISON AMWAGA UGALI SIMBA...ADAI CHANZO CHA KUSIMAMISHWA NI BARBARA..."WACHEZAJI WANAHASIRA"...