Home news BAADA YA KUIONA YANGA NA FUJO ZAO…TRY AGAIN AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA…

BAADA YA KUIONA YANGA NA FUJO ZAO…TRY AGAIN AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA…


SIMBA wamesisitiza kwamba huu ni msimu wao wa mataji kwani kikosi chao kimeiva kuliko misimu minne iliyopita.

Simba imetwaa mataji minne mfululizo msimu uliopita la Ligi Kuu Tanzania Bara na mawili mfululizo ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC) pamoja na Ngao ya Jamii huku watani zao Yanga wakiambulia patupu na kuamua kusajili kwa hasira msimu huu.

Kama Yanga wanadhani mambo yameisha, basi pole yao kwani mabosi wa Simba wametamba kuwa hata msimu huu, wamepania kubeba mataji yote matatu wakianza na Ngao ya Jamii watakaovaana na watani wao katika mechi inayosubiriwa kwa hamu itakayopigwa Septemba 25.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alilisema hata msimu huu, Yanga watulie tu kwani wamejipanga kuhakikisha hawaachi kitu na wanamaanisha wanachokisema.

Try Again alisema Simba imejipanga kuhakikisha inatimiza malengo yake ambayo imejipangia katika msimu huo ujao iwe zaidi ya uliopita na sasa breki ya kwanza kimataifa ni kwenye nusu fainali ya Afrika.

“Hakuna tunachoshindwa kukifanya, malengo yetu msimu huu ni yale yale kama ya msimu uliopita, tunahitaji kuyatetea makombe yetu hayo na uwezo tunao na wachezaji wetu wana kiu ya kuyapambania, tukutane uwanjani,” alisema Salim ambaye si mzungumzaji sana.

Aidha Salim alisema kila jambo linakuja kwa maandalizi kwani Simba imefanya maandalizi makubwa mpaka kufikia hatua kubwa ambayo inaifikia hivi sasa ndio maana wakaenda Morocco ambako ndiko kwenye hadhi yao na sasa wanajiandaa kuanza kambi nyingine nje ya Dar kwa msimu mpya.

Try Again alisema, kwa namna ambavyo wamesajili wachezaji kwa mahitaji muhimu watafikia malengo makubwa waliyoyapanga. 

SOMA NA HII  MBUNGE AMGEUKIA MO DEWJI...ANATAKA APIGIWE MAGOTI NA SIMBA...ISHU NZIMA HII HAPA