Home Habari za michezo KAPOMBE NA CHAMA WAZAMISHA JAHAZI LA SIMBA…WYDAD WASONGA MBELE

KAPOMBE NA CHAMA WAZAMISHA JAHAZI LA SIMBA…WYDAD WASONGA MBELE

Habari za SImba SC

Dakika 90 zimemalizika katika dimba la Mohamed V nchini Morocco kati ya Wydad AC dhidi ya miamba ya soka Tanzania, Simba SC huku Wydad Casablanca wakifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mabingwa Barani Afrika baada ya kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Katika mchezo huo uliokuwa mgumu na wa aina yake huku ukichagizwa na wingi wa mashabiki waliofurika kushuhudia mtanange huo, Wydad wameibuka na ushindi wa bao 1-0 kupitia kwa mshambuliaji wao kinara Bouly Junior Sambou raia wa Senegal dakika ya 24 ya mchezo huo, bao lililodumu mpaka kipyenga cha mwisho cha mwamuzi.

Bao hilo halikuwahakikishia Wydad kusonga mbele, kwani mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Mkapa Jumapili iliyopita, Simba aliibuka na ushindi wa bao 1-0, hivyo kwa matokeo ya jumla baada ya mchezo wa leo yakawa Wydad 1-1 Simba, jambo ambalo kwa kanuni za mashindano hayo, walilazimika kwenda kwenye mikwaju ya penati moja kwa moja ili kutafuta mshindi badala ya kuongezewa dakika 30.

Katika changamoto ya mikwaju ya penati, Wydad weshinda penati nne dhidi ya penati tatu za Simba huku wachezaji wa Simba, Shomari Kapombe na Clatous Chama wakikosa penati zao ambazo zilitua salama mikononi mwa mlinda mlango wa Wydad, Yousef El Mutie.

Huu ni msimu wa tano kwa Simba wakiishia katika hatua ya Robo fainali ya michuano ya CAF (CAFCL na CAFCC) wakati Wydad Casablanca ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mabingwa Afrika, wamekuwa wakitinga hatua ya nusu fainali kila mwaka tangu mwaka 2018.

Wydad sasa watakutana kwenye hatua ya nusu fainali na mshindi kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na CR Belouizdad.

SOMA NA HII  WAMEJILETA,... WACHEZAJI YANGA WATENGEWA MIL 200 KUIUA SIMBA