Home Habari za michezo KOCHA MPYA SIMBA AZIDI KUKINUKISHA CAF….’AJIOKOTEA MAUJIKO’ KAMA YOTEE…

KOCHA MPYA SIMBA AZIDI KUKINUKISHA CAF….’AJIOKOTEA MAUJIKO’ KAMA YOTEE…

Habari za Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amepenya katika orodha ya makocha watatu bora wanaowania tuzo za CAF 2023.

Ikumbukwe kuwa kocha huyo ni mrithi wa mikoba ya Roberto Oliveira aliyefutwa kazi kutokana na kupoteza mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya watani wa jadi Yanga.

Oliveira alikuwa shuhuda ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga ambapo bao la Simba lilifungwa na mshambuliaji Kibu Dennis dakika ya 8 aliposawazisha bao la Kennedy Musonda alyefunga bao dakika ya tatu.

Tuzo hizo za CAF zitafanyika Jumatatu Desemba 11. Benchikha anachuana na Walid Regraui WA Morocco na Alidu Cisse wa Senegal ambaye anapewa chapuo kubwa la kusepa na tuzo hiyo.

SOMA NA HII  BAADA YA 'KUBONDWA' NA ZAMBIA JUZI....TWIGA STARS WARUDI KWA HASIRA...'WAIFUMUA' MALAWI BILA HURUMA...