Home Habari za michezo STAA WA KAGERA SUGAR AZITIA WAZIMU TIMU ZA WAZUNGU ULAYA…BALAA LAKE SIO...

STAA WA KAGERA SUGAR AZITIA WAZIMU TIMU ZA WAZUNGU ULAYA…BALAA LAKE SIO POA AISEE…

Tetesi za Usajili Bongo

Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Anuary Jabir aliyeko nchini Ubelgiji kwa ajili ya majaribio kwenye klabu ya KAA Gent huenda akapata dili la kucheza Ulaya msimu ujao kutokana na baadhi ya timu kuhitaji saini yake.

Nyota huyo aliondoka Aprili mwaka huu kwa ajili ya majaribio ya wiki tatu ingawa kiwango anachoendelea kukionyesha kimemfanya kuendelea kusalia humo huku baadhi ya timu mbalimbali zikianza kumnyatia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Ally Masoud alisema hadi sasa maendeleo ya nyota huyo ni mazuri na kama mambo yataenda vizuri basi huenda akaendelea kusalia huko.

“Kuna timu mbalimbali za Croatia, Uholanzi, Jamhuri ya Czech na Ubelgiji aliyopo ambazo zimeonyesha nia ya dhati ya kumuhitaji kwa ajili ya msimu ujao ingawa mazungumzo nao bado yanaendelea,” alisema.

Kwa upande wa Anuary akizungumza  kutoka Ubelgiji alisema atahakikisha anaendelea kutumia vizuri nafasi aliyoipata kwani malengo yake ni kuona anacheza kwenye nchi ambazo zimeendelea kisoka.

“Nikiwa kama kijana lazima nionyeshe nina nia ya kufika mbali zaidi ya nilipotoka hivyo naamini licha ya tu ya uwezo wangu na umri nilionao ila ninahitaji kuongeza jitihada ili kufikia malengo yangu,” alisema.

Anuary hadi anaondoka Aprili mwaka huu tayari alikuwa ameifungia Kagera Sugar mabao matano ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  AL AHLY ATAKUBALI KUENDELEZA UTEJA DHIDI YA SIMBA LEO AFL