Home Uncategorized UJUMBE HUU HAPA WA SALEH JEMBE KWA MASHABIKI WA SIMBA LICHA YA...

UJUMBE HUU HAPA WA SALEH JEMBE KWA MASHABIKI WA SIMBA LICHA YA KICHAPO MBELE YA YANGA WALIJITOKEZA TAIFA

UJUMBE huu kwa mashabiki wa Simba na Yanga kutoka kwa Saleh Jembe:- Hongera sana mashabiki wa Simba, kwani licha ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa watani wenu Yanga lakini mmechangia kwa kiasi kikubwa kuandika rekodi ya kujaza watu wengi zaidi mwenye uwanja wa Taifa.

Mashabiki wa Simba ndio waliojitokeza kwa wingi zaidi katika mechi hiyo na hii rekodi inawahusu. Hongera pia mashabiki wa Yanga ambao kwa 30 hadi 38% pia mlijitokeza Taifa siku hiyo mkiwa wenyeji, lakini NISISITIZE, si sawa na haitakiwi watu kuendelea kuhujumu mapato kwa kuwa wanakuwa wanahujumu mapato ya hizi klabu lakini Serikali pia.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAUMIZWA NA KUVULIWA UBINGWA WA MAPINDUZI