Home Habari za michezo MOSES PHIRI AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE ZAMBIA…MENEJA WAKE AFUNGUKA TIMU ATAKAYOICHEZEA TZ…

MOSES PHIRI AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE ZAMBIA…MENEJA WAKE AFUNGUKA TIMU ATAKAYOICHEZEA TZ…


MSHAMBULIAJI wa Zanaco FC ya nchini Zambia, Moses Phiri, rasmi ameaga ndani ya timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ambaye anawindwa na timu za Simba na Yanga, amekuwa katika kiwango bora ndani ya timu hiyo jambo ambalo limepelekea timu hizo kumuwania vikali.

Akizungumza moja kwa moja kutoka nchini Zambia, meneja wa mchezaji huyo, Nyambe Nawa, alisema msimu ujao kuna asilimia kubwa kwa Phiri kucheza Tanzania baada ya kuhitajika na timu za Simba na Yanga.

“Simba na Yanga zote zinamuhitaji Phiri, hivyo mpaka sasa kuna asilimia kubwa sana kwake kucheza soka Tanzania msimu ujao, dirisha la usajili likifunguliwa kila kitu kitakuwa wazi,” alisema meneja huyo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA...KAPAMA AWAPIGA 'MKWARA WA KWENDA' MASTAA WENZAKE MSIMBAZI...